MRADI WA SUSWA

Matazamio ya Suswa yana uwezekano wa kutoa takriban megawati mia saba na hamsini (750MW) ambao itazalishwa kwa awamu. Awamu tatu za kwanza zitastawisha jumla ya megawati mia tatu (300MW), na kila moja itastawisha megawati mia moja (100MW). Uchunguzi mahsusi wa eneo la juu la ardhi ulikamilika mapema 2013.
Upataji wa Leseni ya Ukadiriaji Athari za Kimazingira na Kijamii (ESIA) kutoka kwa NEMA unaendelea. Mfumo wa ushirikishaji jamii umeanzishwa.