Hadithi Yetu

Kampuni ya Ustawishaji Kawi ya Mvuke (GDC) ni kampuni inayomilikiwa kikamilifu na serikali katika Sekta ya Nishati ya Kenya. GDC iliundwa mnamo 2008 kama Chombo Maalum (Special Purpose Vehicle - SPV) ili kuharakisha ustawishaji rasilimali za kawi-mvuke nchini Kenya.
GDC imepewa jukumu la kustawisha viwanja vya mvuke na kuuza kawi-mvuke ya kuzalisha umeme kwa Kenya Electricity Generating Company (KenGen) na Wazalishaji Huru wa Nishati (IPPs). Mvuke unaotoka ardhini haudhuru mazingira na ni malighafi inayopatikana kwa wingi inayoweza kutumiwa kuzalisha umeme.
Serikali na washirika wake kadhaa wa maendeleo wamekuwa wakifadhili suluhu dhidi ya hatari zinazohusiana na utafutaji wa kawi-mvuke na uchimbaji visima

Wajibu wa GDC

Kuondoa hatari za awali na kupunguza gharama kupitia ukuzaji wa miundomsingi, kazi za uchunguzi na uchimbaji wa jotoardhi

Kukuza matumizi ya moja kwa moja ya rasilimali za jotoardhi


Kukuza nguvu-kazi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya jotoardhi


Kusaidia washikadau wa sekta binafsi kujiunga na sekta ya jotoardhi, na kuuza mvuke kwa wazalishaji wa nishati

Kusaidia Serikali ya Kenya katika kutafuta ufadhili wa kuendeleza miradi ya jotoardhi


Uzalishaji wa umeme wa mapema kwa kutumia mitambo midogo ya kuzalisha umeme moja kwa moja katika visima vya jotoardhi

HATUA KUU

2009
Mwanzo

GDC kufungua ofisi zake, kuwaajiri wafanyikazi na kuanza kuchimba visima Olkaria

2010
Rigs

Kununuliwa kwa rig mbili za kwanza

2011
Kisima cha kwanza

Kisima cha kwanza huko Menengai, MW-01, ikithibitisha uwepo wa mvuke shambani. Kisima kina uwezo wa 12.5MW

2012
Msaada

Tukapokea msaada kutoka kwa wenzi wetu kukuza Mradi wa Menengai Gethermal

2013
Uwezo

Utafiti wa uwezekano wa Mradi wa Menengai Gethermal

2014
30MW

Kuchimbwa kwa kisima cha 30MW huko Menengai na ununuzi wa rigs za ziada

2015
Direct Use

Launched direct-use pilot projects at Menengai which include a Geothermal Powered Dairy Unit, Geothermal Powered Laundry, Geothermal Heated Aquaculture Ponds and Geothermal Heated Green Houses

2016
Revenue

Earned revenue from steam sales worth approximately Kes 3B from the Olkaria Geothermal Project in Naivasha

2017
North Rift

Kickstarted infrastructure works in the North Rift regions in order to lay the foundation for the development of the Baringo-Silali Geothermal Project

2018
Rig Move

Carried our the first rig move to the Baringo-Silali Project to kickstart the drilling process and completed the construction of the Steam Gathering System for Menengai 105MW