MRADI WA OLKARIA

Uuzaji wa mvuke katika Mradi wa Olkaria

Kufuatia ombi la serikali ya Kenya, GDC mnamo mwaka wa fedha 2009/10 ilichimba visima 36 vya mvuke kule Olkaria. GDC pia ilirithi visima 23 vilivyochimbwa na serikali kabla ya kuianzishwwa kwa GDC, na kufikisha 59 idadi ya visima vyote vinavyomilikiwa na GDC huko Olkaria. Mradi wa Kawi-Mvuke wa Olkaria unamilikiwa na kusimamiwa na KenGen.
Visima 59 vya mvuke vya GDC katika Olkaria vinatoa jumla ya megawati mia nne na kumi na mbili (412MW). GDC inauza megawati mia tatu na ishirini (320MW) ya mvuke kwa KenGen kwa uzalishaji umeme, inapata mapato ya kila mwaka ya Shilingi bilioni tatu (3). Kwa kutoa mvuke wa uzalishaji wa umeme, GDC imesaidia kuondoa utumiaji mitambo ya dizeli ambayo hutoa umeme ghali na unaothiri mazingira.
Kuongezeka kwa megawati mia tatu na ishirni (320MW) za umeme kwa gridi ya kitaifa ya Kenya kumepunguza gharama ya umeme kwa asilimia ishirini na mbili na thelathini na tano (22% na 35%) kwa watumiaji wa majumbani na viwandani mtawalia, na hivyo kusaidia serikali kufikia lengo lake la kutoa nishati ya kijani ya bei ya chini na yenye kuaminika.