MRADI WA MENENGAI

Mradi wa Uzalishaji Mvuke wa Menengai unastawishwa katika awamu nne kila moja ikiwa ya takriban megawati mia moja (100MW). Uwezo wa utoaji wa Mradi wa Uzalishaji Mvuke wa Menengai ni megawati elfu moja mia sita (1600MW).

Awamu ya kwanza ya mradi huo ilianza mnamo Februari, 2011. GDC ina mitambo saba (7) ya kuchimba visima ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa KiKenya kwa kuchimba visima vya mvuke.

Kufikia sasa GDC imepata megawati mia moja sabini (170MW) za mvuke kwenye kichwa cha kisima. GDC imeweka kandarasi tatu (3) na IPP (wazalishaji huru wa umeme) kujenga mitambo mitatu ya kuzalisha umeme chini ya Awamu ya kwanza ya Menengai.