KAMATI YA UTENDAJI

 • Eng. Jared O. Othieno
  Mkurugenzi Msimamizi na Afisa Mkuu Mtendaji

  Mhandisi Jared O. Othieno ndiye Mkurugenzi Msimamizi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Ustawishaji Kawi-Mvuke (GDC). Yeye ni mwanachama wa Tasisi ya Wahandisi wa Kenya (IEK). Ana ujuzi wa uongozi na usimamizi wa zaidi ya miaka 25 katika Sekta ya Nishati na na amehudumu katika nyadhifa tofauti katika Kampuni ya Umeme na Mwangaza Nchini - Kenya Power. Mhandisi Othieno ana tajriba kubwa katika uhandisi wa umeme, mikakati ya kibiashara na usimamizi wa utendaji, michakato ya kibishara, utawala wa shirika, na usimamiaji miradi. Yeye ni mhandisi mtaalam aliyesajiliwa anayeshikilia Shahada ya Uzamili ya Udhibiti wa Biashara (MBA) na Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc) katika Uhandisi wa Umeme kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

 • Bi Beatrice Kosgei
  Meneja Mkuu: Masuala ya Kisheria na Katibu wa Kampuni

  Bi. Beatrice Kosgei ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na Katibu wa Umma Msajiliwa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika shughuli za kisheria na maswala ya kampuni. Hapo awali aliwahi kuwa Katibu wa Kampuni na Mkuu wa Masuala ya Kisheria katika Shirika la Mtandao wa Biashara Nchini (KenTrade).

 • Bwana Cornel Ofwona
  Meneja Mkuu: Ustawishaji Rasilimali ya Kawi-Mvuke

  Bwana Cornel Ofwona ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika tasnia ya kawi-mvuke. Ana utaalam mkubwa katika uhandisi, uchambuzi na ufumaji hifadhi asilia za kawi mvuke. Kabla ya kuteuliwa kwa wadhifa huu, alikuwa Kaimu Meneja Mkuu wa GDC anayesimamia Uchimbaji na Miundombinu. Yeye ndiye Mhandisi wa kwanza wa Hifadhi asilia za Kawi barani Afrika.

 • Bwana Simon Kiplang’at
  Meneja Mkuu: Wafanyakazi na Utawala

  Bwana Simon Kiplang'at ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika usimamizi wa kishirika na uongozi katika sekta za umma na za binafsi. Kabla ya kujiunga na GDC, alikuwa Meneja Mkuu Msaidizi wa Huduma za Wakala wa Biashara wa Kenya (KenTrade).

 • Dkt George Muia
  Meneja Mkuu: Mikakati, Utafiti na Ubunifu

  Dkt. George Muia ni mtaalam wa jiolojia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mazingira ya jiolojia. Hapo awali, alikuwa Msaidizi wa Mkurugenzi Utafiti na Ubunifu katika Kituo cha Mafunzo cha Kampuni ya bomba la Kenya, Kenya Pipeline, Taasisi ya Mafuta na Gesi ya Morendat.

 • Eng. George Kinyanjui
  Meneja Mkuu: Kuchimba na Miundombinu

  Mhandisi George Kinyanjui ana uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya nishati. Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Meneja wa GDC wa Udhibiti Ubora na Usalama.

 • Bi Joanne Wamuyu
  Meneja Mkuu: Huduma za kampuni

  Bi Joanne Wamuyu ni Muuzaji Msajiliwa mwenye sifa na uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika maendeleo ya kibiashara, ushirika na ustawishaji mikakati. Kabla ya kujiunga na GDC, hapo awali alikuwa akisimamia Uuzaji wa Afrika Mashariki kabla ya kuchukua jukumu la ukuzaji wa ujuzi wa kiufundi kote Afrika katika kampuni ya IBM.

 • Bwana Stephen Busieney
  Meneja Mkuu: Fedha

  Bwana Stephen Busieney ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika Fedha na Uhasibu. Kabla ya kujiunga na GDC, alikuwa Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya CIMERWA Cement Company, Rwanda.

 • Bwana Paul Ngugi
  Meneja wa Eneo, Bonde la Ufa Kati

  Bwana Paul Ngugi ni Meneja wa Eneo la Bonde la Ufa Kati la GDC. Bw. Ngugi ana uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika ustawishaji biashara ya kawi-mvuke. Kabla ya kuteuliwa, alikuwa Kaimu Meneja Mkuu wa Huduma ya Kiufundi. Yeye ni mwanachama wa Ushirika wa Kawi-Mvuke wa Kenya.

 • Bi Irene Onyambu
  Meneja wa Eneo, Bonde la Ufa Kusini

  Bi. Irene Onyambu ni Meneja wa Eneo la Bonde la Ufa Kusini la GDC. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu. Kabla ya kuteuliwa kwa wadhifa huu, alikuwa Kaimu Meneja Mkuu, Huduma za Rasilmali Watu. Yeye ni mwanachama wa Taasisi ya Usimamizi wa Wafanyakazi (IHRM).

 • Bwana John Lagat
  Meneja wa Eneo, Bonde la Ufa Kaskazini

  Bwana John Lagat ni Meneja wa Eneo, Bonde la Ufa Kaskazini. Pia anasimamia Ukadiriaji Rasilimali ya Kawi Mvuke. Yeye ni mtaalam wa jiolojia mwenye ujuzi mwingi katika teknolojia ya Kawi-vuke unaozidi miaka 23. Yeye ni mwanachama wa Jumuiya ya Kijiolojia ya Kenya na Ushirika wa Kawi-Mvuke wa Kenya.

 • Bi Doris Kyaka
  Meneja wa Mfumo wa Usambazaji

  Bi. Doris Kyaka ni Meneja, Mfumo wa Usambazaji ambaye anaripoti kwa Mkurugenzi Msimamizi na Afisa Mkuu Mtendaji. Ana Shahada ya Uzamilifu ya Usimamizi wa Biashara (EMBA) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) na amehitimu kutoka Taasisi Sajiliwa ya Ununuzi na Ugavi (CIPS, UK). Bi. Kyaka ni mwanachama wa Taasisi ya Kenya ya Usimamizi wa Ugavi (KISM) ambapo hapo awali alikuwa akihudumu katika Bodi ya KISM kwa miaka miwili. Pia aliwahi kuwa mshiriki wa Taasisi Sajiliwa ya Ununuzi na Ugavi (MCIPS).