SEKTA YA NISHATI YA KENYA

Kampuni ya Ustawishaji Kawi Mvuke (GDC) imo ndani ya Wizara ya Nishati (MoE). GDC iliundwa kufuatia kufunguanishwa kwa sekta ya nishati ili kuunda mashirika yanayoangazia hatua tofauti za mlolongo wa thamani kuambatana na Sheria ya Nishati ya 2006. Washirika wote wamepewa majukumu yaliyofafanuliwa wazi.