BODI YA WAKURUGENZI

 • Dkt. Mha. Joseph Njoroge (CBS)
  Wizara ya Nishati

  Dkt. Mha. Joseph Njoroge (CBS), ni Mhandisi wa Umeme Msajiliwa. Tajriba yake ni ya zaidi ya miaka thelathini katika uhandisi wa nguvu za umeme na usimamizi. Yeye ni mwanachama wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia ya Uingereza, mhandisi wa ushauri aliyesajiliwa, mshiriki wa Taasisi ya Wahandisi wa Kenya (IEK) na mwanachama wa Taasisi ya Wakurugenzi (Kenya).

 • Bwana John Njiraini
  Mwenyekiti (Mkurugenzi Huru asiyehusika na utendaji)

  Bwana John Njiraini ni mtaalam tajika aliye na uzoevu mkubwa wa kuhudmu katika mashirika akiwa amehudumu katika ngazi mbali mbali za kimkakati ikiwa ni pamoja na kama Afisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu wa Umma Waliosajiliwa wa Kenya (ICPAK), na Kamishna wa Ushuru wa Ndani na Ofisi ya Walipa Ushuru Wakubwa katika Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) ambapo alipanda ngazi na hatimaye kuwa Kamishna Jenerali. Ana Shahada ya Biashara (B.Com) na MBA kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

 • Eng. Jared O. Othieno
  Mkurugenzi Msimamizi na Afisa Mkuu Mtendaji

  Mhandisi Jared O. Othieno ndiye Mkurugenzi Msimamizi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Ustawishaji Kawi-Mvuke (GDC). Yeye ni mwanachama wa Tasisi ya Wahandisi wa Kenya (IEK). Ana ujuzi wa uongozi na usimamizi wa zaidi ya miaka 25 katika Sekta ya Nishati na na amehudumu katika nyadhifa tofauti katika Kampuni ya Umeme na Mwangaza Nchini - Kenya Power. Mhandisi Othieno ana tajriba kubwa katika uhandisi wa umeme, mikakati ya kibiashara na usimamizi wa utendaji, michakato ya kibishara, utawala wa shirika, na usimamiaji miradi. Yeye ni mhandisi mtaalam aliyesajiliwa anayeshikilia Shahada ya Uzamili ya Udhibiti wa Biashara (MBA) na Shahada ya Kwanza ya Sayansi (BSc) katika Uhandisi wa Umeme kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

 • Bwana Joseph Waruiru
  Mkurugenzi (Mbadala wa Waziri, Hazina ya Kitaifa)

  Bwana Joseph Waruiru ni mkurugenzi mbadala wa Katibu wa Hazina ya Kitaifa ya Hazina. Yeye ni Mhasibu wa Hesabu za Umma Msajiliwa aliye na ujuzi wa zaidi ya miaka 12 ya ukaguzi katika Huduma ya Umma. Kwa sasa Bw Waruiru anafanya kazi katika Idara ya Uwekezaji wa Serikali katika Biashara, Hazina ya Kitaifa.

 • Dkt Nelly Yatich
  Mkurugenzi Huru asiyehusika na Utendaji

  Daktari Nelly Yatich ni Mtaalam wa Ufuatiliaji, Utafiti wa Kusoma na Tathmini. Dk. Yatich ana shahada ya udaktari katika Afya ya Umma hususan Elimu ya Mlipuko wa Magonjwa kutoka Chuo Kikuu cha Alabama huko Birmingham, Mariakani. Dk Yatich ana tajriba pana katika elimu ya mlipuko wa magonjwa, uchunguzi na tathmini, utafiti wa kimatibabu, uundaji mipango na utekelezaji wake, uandishi wa barua za ruzuku, bajeti na ujenzi wa uwezo. Hapo awali alifanya kazi kama Mkurugenzi wa Nchi katika Chuo Kikuu cha Washington, ambapo alisimamia mipango yote na shughuli za utafiti nchini Kenya. Yeye ni mwanachama wa Muungano wa Afya ya Umma wa Amerika, Jumuiya ya Kimataifa ya Magonjwa ya Kuambukiza, Baraza la Afya Ulimwenguni, na Jamii ya Heshima ya Phi Beta Delta kwa Wasomi wa Kimataifa na Jumuiya ya Heshima ya Delta Omega katika Afya ya Umma.

 • Bwana Mwendia Nyaga
  Mkurugenzi Huru asiyehusika na Utendaji

  Bwana Mwendia Nyaga ndiye mwanzilishi na mshauri anayeongoza katika kampuni ya huduma za mafuta na nishati – Oil and Energy Services Limited. Ana uzoefu wa miaka 15 kwenye tasnia ya mafuta na gesi. Mtaalam wa petroli na fedha mwenye uzoefu wa kuishauri Serikali ya Kenya kuhusu shughuli za kwanza katika utoaji mafuta na gesi, Mwendia anaelewa kwa kina mahitaji ya mwekezaji na ya serikali katika sekta hii na anajihusisha hasa na kusaidia wateja kupenya sekta hii inayochipuka. Mwendia ni mtaalam wa ushirikishwaji na unufaishaji wenyeji katika sekta hii nchini akiwa amechangia pakubwa katika mazungumzo juu ya maendeleo endelevu yanayohusiana na ustawishaji uhusishwaji wenyeji katika miradi Afrika Mashariki

 • Bi Anne Too
  Mkurugenzi Huru asiyehusika na Utendaji

  Bi Anne Too amefanya kazi kama mshauri katika ofisi ya Naibu Spika wa Bunge. Bi Too pia aliwahi kuwa mshauri wa kibinafsi katika ofisi ya Waziri Msaidizi, Masuala ya Humu Nchini. Ana ustadi bora wa usimamizi na mawasiliano. Hujisukuma mwenyewe pia na hushiriakana na anaofanya kazi nao. Ana Shahada ya Saikolojia na Elimu ya Jinai kutoka Chuo Kikuu cha Keele, Uingereza.

 • Bwana Kamau Kuria
  Mkurugenzi Huru asiyehusika na Utendaji

  Bw Kamau Kuria ni mjasiriamali wa kijamii na kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Afrikaqua Limited na Mwenyekiti wa Ikotoilet Limited.Ana shahada yakKwanza ya Usanifu Majengo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) na Shahada ya Uzamili katika Uendeshaji Biashara kutoka Chuo Kikuu cha KCA. Anakamilisha masomo yake ya Shahada ya Udaktari (PhD) katika Usimamizi wa Miradi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT). Yeye ni mwanachama wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi-Uingereza. Bw Kuria amepokea tuzo nyingi katika ujasiriamali wa kijamii. Tuzo hizo ni pamoja na Mjasiriamali wa Kijamaa wa Afrika Mwaka wa 2009 (Jukwaa la Uchumi Duniani Davos, Uswizi) Ushirika wa Ashoka, Ushirika wa Aspen na Ushirika wa Schwab. Amewahi kuwa mjumbe wa Baraza la Ujasiriamali la Ajenda ya Kimataifa, Ushirikiano wa Sekta Binafsi ya Kenya, Maji, Mazingira na Jopokazi la Maliasili, Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki na Kamati Kuhusu Viwango vya Ubora wa Majitaka ya Shirika la Kukadiria Ubora la Kenya. Bw Kuria pia ni mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Wanafunzi Waliopitia Shule za Kenya.

 • Bwana Namada Simoni
  Mkurugenzi Huru asiyehusika na Utendaji

  Bwana Namada Simoni ni wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 20 wa kuhudumu katika nyanja ya sheria. Kwa sasa yeye ndiye Mshirika Mkuu huko Namada & Co Advocates. Yeye ni Mwanachama wa Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK) na Chama cha Wanasheria ya Afrika Mashariki (EALS).