MRADI WA BARINGO-SILALI

Kampuni ya Ustawishaji Kawi-Mvuke (GDC) inachangia mno katika maendeleo ya jamii wenyeji. Tunafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na jamii wenyeji kuhakikisha mahusiano mema yanaanzishwa na kutunzwa kwa faida ya pande zote mbili. Msaada wa GDC kwa jamii hizi unaongozwa na mahitaji wanayoyahisi katika nyanja za elimu; afya, uwezeshaji wa kiuchumi; usimamizi wa mazingira na pia katika kuunga mkono sanaa, utamaduni na michezo.

Baadhi ya shughuli ambazo GDC imefanya kwa faida ya jamii na mazingira ni pamoja na:
Kipande cha ardhi cha Baringo-Silali kina uwezo wa utoaji takriban megawati elfu tatu (3,000MW) ambao utastawishwa kwa awamu. Awamu tatu za kwanza zitastawisha megawati mia moja (100MW) kutokana na ufadhili kutoka kwa Serikali ya Kenya na shirika la Ujerumani la KfW. Uchunguzi wa kina ulikamilika mapema 2013 na Leseni ya Ukadiriaji Athari za Kimazingira na Kijamii (ESIA) ilipatikana kutoka kwa NEMA. Mfumo wa kushirikisha jamii umeanzishwa na jamii imeipa GDC haki ya kufikia ardhi hiyo.

Serikali ya Kenya (GoK) inafadhili ujenzi wa barabara za kuelekea kwa mradi na mipango ya kushirikisha jamii wakati ambapo KfW imeipa GDC mkopo nafuu wa Euro Milioni 80, takriban Sh.8 bilioni, kwa kuchimba visima 15 hadi 20 vya mvuke, kupokea ushauri kadhaa wa kitaalam na kuweka bomba la maji ili kusambaza maji ya kutumika kuchimba visima.

Kufikia sasa, GDC imekamilisha barabara zinazoelekea kwenye mradi, ambazo ni zaidi ya kilomita mia moja (100km), kufungua eneo la Baringo-Silali liweze kuchimbwa. Kuchimba kulianza Desemba 2018.