Green Energy For Kenya

Kampuni ya Ustawishaji Kawi ya Mvuke (GDC) ni kampuni inayomilikiwa kikamilifu na serikali katika Sekta ya Nishati ya Kenya. GDC iliundwa mnamo 2008 kama Chombo Maalum (Special Purpose Vehicle - SPV) ili kuharakisha ustawishaji rasilimali za kawi-mvuke nchini Kenya. GDC imepewa jukumu la kustawisha viwanja vya mvuke na kuuza kawi-mvuke ya kuzalisha umeme kwa Kenya Electricity Generating Company (KenGen) na Wazalishaji Huru wa Nishati (IPPs). Mvuke unaotoka ardhini haudhuru mazingira na ni malighafi inayopatikana kwa wingi inayoweza kutumiwa kuzalisha umeme. Serikali na washirika wake kadhaa wa maendeleo wamekuwa wakifadhili suluhu dhidi ya hatari zinazohusiana na utafutaji wa kawi-mvuke na uchimbaji visima

DIRA

Kustawisha nishati mbadala kwa Kenya kutoka kwa rasilimali za kawi-mvuke

DHIMA

Kuwa kiongozi ulimwenguni katika ustawishaji rasilimali za kawi-mvuke

MAADHILI MSINGI

Uadilifu
Utaalam

Mamlaka

Kukuza ustawishaji wa haraka wa rasilmali ya kawi-mvuke nchini Kenya kupitia utafutaji wa ishara za juu ya ardhi za uwepo wa kawi mvuke na kuchimba visima ili kupata mvuke.

Kuwapa mvuke watengenezaji wa mitambo ya umeme kwa uzalishaji wa umeme

Kusimamia hifadhi asilia za kawi-mvuke ili kuhakikisha ugavi thabiti wa mvuke kwa uzalishaji umeme

Kukuza matumizi mbadala ya rasilmali za kawi-mvuke kando na uzalishaji umeme pekee. Hii ni pamoja na kupasha joto nyumba za kioo za kukuzia mimea, kukausha nafaka, kuondoa vijidudu kwenye maziwa, kupasha joto na kupoza vyumba, miongoni mwa mengine.